Nyumba ya Roho Lyrics

NYUMBA YA ROHO

@ Charles Ruta

Mungu wangu nikujue mimi, Mungu wangu nikupende
Mungu nikutumikie, kisha niurithi ufalme Mbinguni * 2
(wewe) roho umenipa ee, (kisha) ukaihifadhi vizuri
(yaani) ndani ya mwili ee (kwani) mwili ni nyumba ya rho

 1. Ndiwe mungu peke yako, wa kuabudiwa ni wewe
  Nishike kitakatifu siku hiyo siku yako
  nisilitaje kabisa bure jina lako Mwenyezi
  Ulimi wa mwili wangu usiiponze roho yangu
 2. Niwaheshimu wazazi, ili nisiwasononeshe
  Uhai wa binadamu niuthamini yani nisiuue
  Kuiba nijiepushe, kusema uwongo niache
  Mwili wangu usizini ndipo roho yangu itapona
 3. Niepuke kutamani yote yasiyo mali yangu
  Naye mwanamke asiye mke wangu yani sio wangu
  Hapo ndipo nitakuwa nimeutumia vizuri
  Mwili ulioiumbia roho ifike Mbinguni juu
Nyumba ya Roho
COMPOSERCharles Ruta
CHOIRSt. Kizito Makuburi
ALBUMNyumba ya Roho
CATEGORYRoho Mtakatifu (Pentecoste)
 • Comments