Kipeperushe Kitambaa Chako

Kipeperushe Kitambaa Chako
Performed by-
CategoryUbatizo
Views8,777

Kipeperushe Kitambaa Chako Lyrics

  1. [ t ] Jiangalie jinsi unavyoenenda,
    ujiulize kama hivyo ni sawa
    Ndugu rejea ahadi yako kumkataa Ibilisi muovu
    [ t ] Dhamira yako inakuambia nini,
    inakusuta au bado ni huru, sasa
    Ndugu rejea ahadi yako kumfuata Bwana Yesu milele

    Ewe Mwenzangu - kipeperushe kitambaa chako
    Cha ubatizo - cheupe kinachomeremeta
    Kisichafuke - kipeperushe kitambaa chako
    Cha ubatizo - cheupe kinachomeremeta
    Kiweke safi - kipeperushe kitambaa chako
    Cha ubatizo - cheupe kinachomeremeta

  2. Uliye naye kweli ni mzuri sana,
    pia kumbuka yuko wako wa ndoa -
    Uliyeapa ni wewe sio mwingine,
    kushikamana naye yule mmoja, basi -
  3. Maendeleo kweli ni muhimu sana,
    lakini na wenzako wanahitaji -
    Hicho kipato ndicho ulichopimiwa,
    au mwenzetu unachota zaidi, leo -
  4. Unatamani kuwa mwenye madaraka,
    umejiandaaje kuyatumia -
    Je ni halali watu tukakutukuza,
    wakati yupo yule alokuumba, haya -
  5. Kumbuka Yesu alipigwa mijeredi,
    kwa sababu ya haya unayotenda -
    Akatundikwa mtini akiwa tupu,
    kadhalilishwa mwisho akauawa, hivyo -
  6. Kumbuka kuwa siku ile inakuja,
    matendo yako yote kuhesabiwa -
    Ni heri leo ukitunze kitambaa,
    siku ya mwisho kiwa bado cheupe, kweli -