Sadaka ya Uchungu

Sadaka ya Uchungu
Performed by-
CategoryFaith
ComposerVictor Aloyce Murishiwa
Views6,125

Sadaka ya Uchungu Lyrics

  1. { Sadaka ya uchungu na kitubio cha machozi
    Vitanifaa nini kama nisipolainisha moyo } *2

  2. Moyo wangu mgumu tena mgumu kama jiwe
    Na kumwagia maji juu ya jiwe kazi bure
  3. Nisipolitangaza pendo la Mungu kwa vitendo
    Kamwe sitazionja baraka na rehema zake
  4. Na nisipoikiri kanuni ile ya imani
    Hata nikeshe mimi kwa maombi ni kazi bure
  5. Ni heri nikubali kikao cha upatanishi
    Nimkane shetani na nguzo zake nizivunje