Imeandikwa Wapi Lyrics

IMEANDIKWA WAPI

@ Victor Aloyce Murishiwa

Nimefungua vitabu vyote nikapekua kurasa zote
Kulitafuta andiko hili sikuliona
Ni wapi palipohalalishwa matendo haya
machafu sana yachafuayo jamii yetu sikupaona
Fungua macho mkristu, fungua macho
Giza nene limetanda, fungua macho
Ni wakati wa kukesha, fungua macho
Shetani katuzunguka, fungua macho
Imeandikwa wapi kwamba ushoga ni halali?
Wapi palipoandikwa rushwa ni funguo ya haki?
(tena) Imeandikwa wapi kwamba hirizi ni halali?
Wapi imehalalishwa wanaume kufunga ndoa?
(hiyo) Imeandikwa wapi, imeandikwa wapi?
Kurasa zote hakuna!
Imeandikwa wapi imeandikwa wapi?
Sheria zake Mungu!

 1. Kemea Mkristu matendo hayo
  Kwa sakramenti zote uyasafishe
  Epukana nayo matendo hayo
  Kwa sakramenti zake uyasafishe
 2. Ingia katika shamba la Bwana
  Mambo ya ulimwengu ni machafuko
  Tembea katika shamba la Bwana
  Zitende kazi zake kwa moyo safi
 3. Njia zake Bwana usiziache
  Ni barabara safi zenye amani.
  Sheria za Bwana usiziache
  Na maagizo yake ni ya Adili
Imeandikwa Wapi
ALT TITLENimefungua Vitabu Vyote
COMPOSERVictor Aloyce Murishiwa
CHOIRSt. Cecilia Mavurunza
ALBUMNimefungua Vitabu Vyote
CATEGORYTafakari
MUSIC KEYKey A
TIME SIGNATURE3
8
NOTES Open PDF
 • Comments