Bwana Ametukuka Sana Lyrics

BWANA AMETUKUKA SANA

@ Renatus Rwelamira

BWANA AMETUKUKA SANA

 1. Ndipo Musa na (wana) wa Israeli
  wakamwimbia Bwana wakinena

  Nitamwimbia Bwana kwa kinywa changu
  Kwa maana ametukuka sana
  Farasi na mpanda farasi amewatupa baharini
  Bwana ni nguvu zangu na wimbo wangu
  Naye amekuwa wokovu wangu
  Yeye ni Mungu wangu na baba yangu nami nitamsifu
 2. Bwana ni mtu wa vita, mtu wa vita
  Bwana ndilo jina lake jina lake
  Magari na jeshi lake Farao amewatupa baharini
  Maakida yake wateule wamezama bahari ya shamu
  Vilindi vimewafunikiza walizama vilindini kama jiwe
 3. Bwana mkono wako wa kuume
  Umepata fahari ya uwezo
  Bwana mkono wako wa kuume wawatesatesa adui
  Kwa wingi wa ukuu wawangusha chini wanaokuondokea
 4. Utawaingiza Bwana na kuwapanda
  Katika mlima wa urithi wako
  Mahali pale ulipojifanyia Bwana ili upakae
  Pale patakatifu ulipopaweka imara Bwana
  Bwana kwa mikono yako
  Bwana atatawala milele yote

  Ndipo Musa…..
Bwana Ametukuka Sana
ALT TITLENitamwimbia Bwana
COMPOSERRenatus Rwelamira
 • Comments