Ee Nafsi Yangu Lyrics

EE NAFSI YANGU

{ Ee nafsi yangu mhimidi Bwana, wewe Bwana Mungu wangu,
umejifanya mkuu sana, umejivika heshima na adhama } * 2

  1. Umejivika nuru kama vazi, umezitandaza mbingu kama pazia
    Na kuziweka nguzo za horofa, nguzo za horofa zake majini
  2. Huwafanya malaika zake, huwafanya kuwa pepo
    Na watumishi watumishi wake, huwafanya kuwa moto wa miali
  3. Ee Bwana jinsi yalivyo mengi, yalivyo mengi matendo yako
    Kwa heshima umefanya vyote, dunia imejaa mali yako
Ee Nafsi Yangu
CHOIRSt. Maurus Kurasini
ALBUMHubirini Kwa Kuimba
CATEGORYZaburi
REFZaburi 104
  • Comments