Nitajisifia Udhaifu Wangu Lyrics

NITAJISIFIA UDHAIFU WANGU

@ Marcus Mtinga

Nitajisifia udhaifu wangu udhaifu wangu,
ili uweza wa Kristu ukae juu yangu
maana ninapokuwa dhaifu ndipo nilipo na nguvu x2

 1. Sina budi kujisifia japo kuwa haipendezi,
  lakini ninajizuia nisihesabiwe hatia,
  bali nasema ukweli juu ya maono niliyopata.
 2. Sababu ya mafunuo hayo nalipewa mwiba mwilini,
  nikamsihi Mungu wangu jambo hili liniepuke,
  naye akaniambia neema yangu pekee inatosha.
 3. Napendezwa na udhaifu dharau taabu mateso,
  nakuyavumilia yote hayo kwa ajili ya Kristu,
  kwani uweza wa Kristu hutimia katika udhaifu.
Nitajisifia Udhaifu Wangu
COMPOSERMarcus Mtinga
CATEGORYTafakari
 • Comments