Dira

Dira
Alt TitleAsipojenga Nyumba
Performed byKwaya ya Malkia wa Mitume Parokia ya Vincent Palloti Arusha
AlbumDira
CategoryTafakari
ComposerBernard Mukasa
Views5,147

Dira Lyrics

  1. Asipojenga nyumba wale waijengao
    wanafanya kazi bure na wanapoteza muda
    Na wanaoulinda mji wanapoteza usingizi
    maana wanakesha bure wao si lolote si kitu
    Hakuna jema nje ya Mungu, hakuna mali pasipo yeye
    Hakuna ushindi bila Mungu wala kufanikiwa asipokuwapo

    {(Yeye) Ni nguzo ya yote, nguzo ya kila kitu
    Ni uwezo wote na sababu ya mema yote
    (Yeye) ni dira (aoh) daima tumtangulize * 2 } *2

  2. Ewe tajiri mali uliyo nayo isalimishe
    mikononi mwake Mungu
  3. Nawe msomi vyeti ulivyo navyo ni vumbi tupi
    kama hujampa Mungu
  4. Ewe mzima, nguvu na afya na uhai ni bure
    Kama havilindi Mungu
  5. Kuumwa kwako na shida zako zitakuangamiza,
    kama hujampa Mungu

    Ni nguzo yetu na dira yetu
    Ni ngao yetu milele