Yesu Njoo Rohoni Mwangu

Yesu Njoo Rohoni Mwangu
Performed byMaria Mt Mama wa Mungu Musoma
AlbumMatumaini ya Safari
CategoryEkaristia (Eucharist)
ComposerD. Kizange
Views9,601

Yesu Njoo Rohoni Mwangu Lyrics

  1. Yesu njoo rohoni mwangu, karibu nakukaribisha
    Naumia rohoni mwangu, njaa kiu vinanitesa
    { Kimbilio langu ni wewe, nimekuja unilishe
    Mwili wako na damu yako, nipate uzima milele } *2
    Yesu njoo rohoni mwangu, nipate faraja milele

  2. Najongea meza yako, japo sifai kabisa
    Wewe wanikaribisha na uovu wangu wote
  3. Yesu wangu nguvu yangu, unilishe mwili wako
    Wewe ndiwe tegemeo la maisha yangu yote
  4. Wewe ndiwe kitulizo cha Roho yangu milele
    Bila wewe sina nguvu roho yangu ni dhaifu
  5. Mwili wako ni chakula damu yako ni kinywaji
    Unilishe uninyweshe siku zote kaa name