Hapa We Msafiri Lyrics

HAPA WE MSAFIRI

@ Fr. G. F. Kayeta

 1. Hapa we msafiri simama na tazama (simama na tazama)
  Nimekufa leo, kesho - ni zamu yako
  (ona) ona vema nilivyowekwa humu,
  Na nilivyoacha mali na jamaa
 2. Nilitoka uchi tumboni mwa mamangu . . .
  Narudia uchi, kati-ka tumbo la nchi
  (Sanda) sanda moja hilo ni vazi langu,
  Wameninyang'anya hata senti moja.
 3. Nifunike vema na hilo jembe lako . . .
  Nalitangatanga, kati-ka ulimwengu
  (Basi) basi leo kiburi kimekwisha,
  Kumbe dunia hii ni mti mkavu.
 4. Nyumba yangu leo ni shimo udongoni . . .
  Hakuna mlango, haku-na madirisha
  (Kita) kitanda changu na blanketi langu,
  Ni udongo mzito wanielemea
 5. Kifafanuacho wafu mbele ya Mungu . . .
  Si cheo kikubwa, si da-raja si sifa
  (Mate-) matendo mema saa ya kufa kwangu,
  Yatafungua mlango wa uwingu
 6. Ole wangu mimi nilifanya ujinga . . .
  Kwa kuambatana, na wa-tu wa dunia
  (Ona) ona wote leo wameniacha,
  Hasa watu wale niliowapenda.
 7. Unapojiona jiwazie mwenyewe . . .
  Kufa siku moja, kwa wo-te ni lazima
  (Japo) japo sultani japo ni mtumwa,
  Mungu atamwita ikiwa saa yake.
 8. Nimekufa leo nilipona salama . . .
  Nalijidhania, mwenye - afya mwilini
  (na ma-) na mara moja nikaanguka chini
  Labda huamini kwamba nali`mzima.
 9. Yesu msalabani kateswa vikali mno . . .
  Kwa kutukomboa, aka-mwaga damuye
  Wahurumie wote wa toharani,
  Mwanga wa milele uwaangazie.
 10. Kwaherini wote kwaherini wapenzi . . .
  Ninakwenda kwetu sita-rudi nyuma
  (Kwa he-) Kwaheri Baba kwaheri Mama yangu,
  Mungu akipenda kwake tukutane.
Hapa We Msafiri
COMPOSERFr. G. F. Kayeta
CATEGORYMazishi
MUSIC KEYB Flat Major
TIME SIGNATURE4
4
NOTES Open PDF
 • Comments