Tutawapeni Mapesa Lyrics

TUTAWAPENI MAPESA

@ A. S. Haule

 • Haya enyi makamanda, leteni mchango wenu *2
  Nguvu ya hoja itawa-ale,
  Hawa walinzi wameleta habari kuwa kweli amefufuka, amefufuka *2
  Sikieni mimi natoa hoja ya nguvu, hoja yangu kweli ya nguvu
  Jambo hili likisikika, likisikika katika Uyahudi
  Na Samaria itakuwaje aibu hiyo elezeni *2

 • Hivyo ninyi walinzi, seme-ni
  Wanafunzi wake wamemwiba Bwana wao *2
  Sisi tulipokuwa tumelala *2
 • { (Tutawapeni mapesa) tutawapeni mapesa,
  Tutawajaza mapesa, mapesa mtajazwa } *2
  Na msiogope kwa ajili ya hilo * 2
  { Wakuu wa nchi wakisikia tutaongea nao
  Wakuu wa nchi hao tutasema nao } *2
 • a. Siku ile ya kufufuka Bwana, maaskari walitetemeka
  Wakaenda kwa upesi kumwona jemedari mkuu kumpasha habari
 • b. Jemedari akafadhaika akawaita watu pamoja kwa shauri;
  Wakafanya shauri juu ya jambo hili lipate sura, sura mpya.
 • c. Dunia yetu siku hizi yafananaje na haya mambo yaliyotokea;
  Ukweli unapindishwa ili lile la uongo liwe kweli
Tutawapeni Mapesa
ALT TITLEHaya Enyi Makamanda
COMPOSERA. S. Haule
CHOIRSt. Charles Lwanga Yombo Dovya Dsm
ALBUMKafufuka Mwokozi
CATEGORYPasaka (Easter)
MUSIC KEYKey G
TIME SIGNATURE2/4
SOURCESt. Theresa Cathedral Arusha Tanzania
NOTES Open PDF


Also recorded by St. Cecilia Arusha
 • Comments