Nikitazama Pande Zote

Nikitazama Pande Zote
Performed by-
CategoryZaburi
ComposerD. Wasonga
Views3,081

Nikitazama Pande Zote Lyrics

  1. Nikitazama pande zote, pande za dunia,
    Nikiinua macho yangu niitazame dunia;
    Naiona kazi tukufu,kazi ya mikono yako *2

  2. Wewe Bwana hakika wavipenda vitu vyote,
    wavipenda vitu vyote, vitu vyote vilivyomo,
    vitu vyote vilivyomo ni kazi yako tukufu
  3. Wala hukichukii chochote ulichokiumba,
    wala hukichukii chochote ulichokiumba,
    kwani hivyo vyote ni kazi ya mikono yako.
  4. Kaskazini na kusini mashariki hata magharibi,
    pande zote za dunia zadhihirisha utukufu wako,
    zadhihirisha utukufu wako,utukufu wa kazi yako
  5. Jinsi jina lako lilivyo tukufu ndivyo kazi
    ya mikono yako ilivyotukuka duniani,
    kazi ya mikono yako imetukuka duniani kote.