Ee Bwana Nifundishe Kupenda

Ee Bwana Nifundishe Kupenda
Performed bySt. Gregory kwa Mrombo
AlbumKanyaga Twende
CategoryTafakari
ComposerBernard Mukasa
Views8,351

Ee Bwana Nifundishe Kupenda Lyrics

  1. Ee Bwana nifundishe kupenda, ee Bwana nifundishe kutumikia
    Ee Bwana nifundishe (kuwajua wenzangu ee) Ee Bwana nifundishe kutumikia

  2. Nifanye juhudi kuwajua watu, kusudi nizifahamu shida zao
    Nisiwape kazi kubwa kutafuta njia ya kunieleza shida zao
    Nisiwe mwenye haraka kuwachoka, niliowasaidia mara nyingi
    Nijue kusaidia ni safari, iliyo na milima mingi na miiba
  3. Nijue kuwatetea wadhaifu, wasipoteze thamani nikiona
    Maana hawakuchagua hali yao. Wamekuwa hivyo kusudi utukuzwe
    Nijibidiishe daima kutafuta, kuwasiliana na jamaa zetu
    Kwa kuwa mahusiano ni gharama, hayawezi kuwepo bila jitihada
  4. Maana nikishajua kupenda, na nikazingatia kutumikia
    Kilicho nileta hapa duniani, kitakuwa kimetia niondoke