Kanisa la Kitume Lyrics

KANISA LA KITUME

@ John Mgandu

Kanisa la kitume (kanisa la kitume)
Kwa sababu Roho Mtakatifu aliwashukia
{ Wale wote waliokuwapo , wale wote waliokuwepo
wakati wa pentekoste wakati wa pentekoste } *2

 1. Asili ya kanisa letu limetoka kwa mitume
  Na limeendelea kukua tangu wakati huo
 2. Huu muungano na mitume unadokeza kwa kanisa
  Kuwa mwaminifu kwa mafundisho
  Yaliyofunuliwa na Yesu na mitume kwetu sisi
 3. Roho Mtakatifu ni mjumbe wa mitume na kanisa
  Atakuwa kati yao kila wakati
  Ni mwalimu wa habari njema aliyoihubiri Yesu
Kanisa la Kitume
COMPOSERJohn Mgandu
CHOIRKwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha
ALBUMKando ya Mito
CATEGORYChurch
MUSIC KEYA Flat Major
TIME SIGNATURE3
8
NOTES Open PDF
 • Comments