Wamegawanyika

Wamegawanyika
Alt TitleNikiiwazia wazia Kazi ya Mwenyezi
Performed byKwaya ya Malkia wa Mitume Parokia ya Vincent Palloti Arusha
AlbumDira
CategoryTafakari
ComposerE. A. Minja
Views4,082

Wamegawanyika Lyrics

  1. Nikiiwaziawazia kazi yake Mwenyezi lo
    Na alivyomuumba huyu mwanadamu
    Tazama inavyopendeza kazi yake Mwenyezi lo
    Na wengine kwa jinsi wanavyojipanga

    { Lakini sasa wamegawanyika
    Tazama leo wao si kitu kimoja } *2

    Wengine wanatafuta upendo ili kuwajali wengine
    Wengine wamefanana na yule simba mnyama mkali
    Wengine watafutacho ni mali tena utu umepotea
    Hakuna kiburi cha kumwaga damu ya watu wengine

  2. Unapowatazama wa nje eeh eeh
    Na kwa jinsi wanavyopendeza eeh eeh
    Hata kwenye miondoko yao eeh eeh
    Wewe mwenyewe utawapenda eeh eeh
    Lakini katika nyoyo zao eeh eeh
    Wako katika sura ya kazi eeh eeh
    Kwa kweli katika roho zao eeh eeh
    Upendo kwao ni kama chambo eeh eeh
  3. Na wengine wanapojipamba eeh eeh
    Utawadhania malaika eeh eeh
    Nyumba magari ya kifahari eeh eeh
    Mwendo wao ni wenye heshima eeh eeh
    Tembea wataongea yao eeh eeh
    Kwa upole upendo amani eeh eeh
    Kumbe moyoni wana kikao eeh eeh
    Leo iwe ni zamu ya nani eeh eeh
  4. Wamezoea kupata mali eeh eeh
    Bila kuwa na moyo wa utu eeh eeh
    Kuwatoa wengine kafara eeh eeh
    Si tatizo bora wafaulu eeh eeh
    Kukata viungo vya wenzao eeh eeh
    Kwao wanachojali ni mali eeh eeh
    Na wengine kufanywa pepeta eeh eeh
    Utu si kitu bora ni mali eeh eeh
  5. Kweli wachuna ngozi wenzao eeh eeh
    Sasa ni zamu ya albino eeh eeh
    Tatizo la yote hayo ni mali eeh eeh
    Pengine watabadili wazo eeh eeh
    Na kusema sasa ni weupe eeh eeh
    Kisha waseme sasa wafupi eeh eeh
    Wataongeza sasa wanene eeh eeh
    Wapate mali kishirikina eeh eeh