Bwana Ndiye Mchungaji Wangu Lyrics

BWANA NDIYE MCHUNGAJI WANGU

@ John Mgandu

{ [ s ] Bwana ndiye mchungaji wangu
[ w ] Bwana ndiye mchungaji wangu
Sitapungukiwa na kitu * 3 } * 2

 1. Bwana ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu
  Katika malisho ya majani mabichi hunila-za
  Kando ya maji ya utulivu hu-niongoza
 2. Huniuhuisha nafsi yangu, na kuniongoza
  Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake
  Nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, sitaogopa mabaya
 3. Huandaa meza mbele yangu, machoni pa watesi wangu
  Hunipaka mafuta kichwani kichwani mwangu
  Na kikombe kikombe changu ki-nafurika
 4. Kwa hakika wema na fadhili zitanifuata
  Siku zote za maisha yangu maisha yangu
  Nami nitakaa nyumbani mwa Bwa-na milele
Bwana Ndiye Mchungaji Wangu
COMPOSERJohn Mgandu
CHOIRSt. Maurus Kurasini
ALBUMHubirini Kwa Kuimba
CATEGORYZaburi
REFZaburi 23
MUSIC KEYB Flat Major
TIME SIGNATURE2
4
SOURCETanzania
NOTES Open PDF
 • Comments