Ee Bwana Ninakuja

Ee Bwana Ninakuja
Performed by-
AlbumKila Kunapokucha
CategoryInjili na Miito (Gospel)
Views4,217

Ee Bwana Ninakuja Lyrics

  1. Ee Bwana ninakuja mbele ya altare yako
    Unipokee Bwana wangu nikutumikie
    Ninajitolea kwako maisha yangu yote
    Nakuomba unitakase niwe mtumishi wako
    Hayana haja ya dunia nikutumikie wewe
    Unijaze roho wako niwe mtumishi mwaminifu

  2. Ninakuja kwako Bwana, unipokee Muumba wangu
    Nahitaji wito ewe Bwana Mungu wangu
    Unijaze roho wako nikutumikie
  3. Bila msaada wako, peke yangu hakika siwezi
    Nahitaji nguvu yako Bwana inisaidie
    Unijaze roho wako nikutumikie
  4. Ni vikwazo vingi sana, vya shetani vinavyonisonga
    Nahitaji neema yako ili nivishinde vyote
    Unijaze roho wako nikutumikie