Nimekutumaini Wewe Lyrics

NIMEKUTUMAINI WEWE

@ Joseph Makoye

Nimekutumaini wewe e Bwana,
nimekutumaini wewe ee Bwana
Nimesema wewe u Mungu wangu,
siku zangu zimo mikononi mwako

  1. Nimekukimbilia wewe ee bwana
    Nisiaibike milele, kwa haki yako yako uniponye
  2. Wewe ndiwe genge langu na ngome yangu
    kwa ajili ya jina lako, uniongoze unichunge
  3. Wewe ni nuru yangu unimulike
    wewe ndiwe wokovu wangu, uniokoe na adui
Nimekutumaini Wewe
COMPOSERJoseph Makoye
CATEGORYZaburi
  • Comments