Ni Mpango wa Mungu

Ni Mpango wa Mungu
Performed by-
AlbumMilele Milele Nitakusifu
CategoryTafakari
Views4,253

Ni Mpango wa Mungu Lyrics

  1. {Ni mpango wa Mungu Baba, kuniumba hivi nilivyo
    Na jinsi alivyoniumba, ili yeye atukuzwe } * 2

  2. Tazama mimi ni kipofu, nawe mwenzangu unaona
    Ni mpango wa Mungu Baba ili kwa hilo atukuzwe
  3. Tazama mimi ni kiwete, nawe mwenzangu watembea
    Ni mpango wa Mungu Baba ili kwa hilo atukuzwe
  4. Tazama mimi ni mweusi, nawe mwenzangu ni mweupe -
    Tazama mimi ni mfupi, nawe mwenzangu ni mrefu -
  5. Tazama mimi maskini, nawe mwenzangu ni tajiri -
    Tazama unao watoto, bali mimi nawatafuta -