Kando ya Mito

Kando ya Mito
Performed byKwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha
AlbumKando ya Mito
CategoryZaburi
ComposerGabriel C. Mkude
Views11,185

Kando ya Mito Lyrics

  1. { Kando ya mito ya Babeli ndiko tulikoketi
    Tukalia tulipoikumbuka kumbuka Sayuni } *2

  2. Katika miti iliyo katikati yake
    Tulivitundika vinubi vinubi vyetu
  3. Maana huko walituchukua mateka
    Na walitaka tuwaimbie nyimbo za Sayuni
  4. Na tuimbeje nyimbo nyimbo zake wa Bwana
    Katika nchi ya ugenini ee Yerusaleme
  5. Ulimi wangu na ugandamane
    Na kaa la kinywa changu nisipokukumbuka