Hii ni Sauti Lyrics

HII NI SAUTI

@ E. F. Jissu

Hii ni sauti ya mtu yule, aliaye kutoka nyikani * 2

Itengezeni njia ya Bwana,yanyoosheni mapito yake * 2
Na wote wenye mwili watauona, wokovu wa Mungu aleluya * 2

 1. Haya ng'oeni magugu yote, tusafishe tusafishe
  Haya ng'oeni na mizizi yake, tusafishe tusafishe
  {Tusaishe bila ya kinyongo, ndugu zangu tusafishe
  Tusafishe kwa moyo mmoja, ndugu zangu tusafishe}
 2. Tuichimbeni mizizi ya rushwa, tusafishe tusafishe
  Tuyafukieni mashimo ya rushwa, tusafishe tusafishe
  Tusafishe bila ya kinyongo, ndugu zangu tusafishe
  Tusafishe kwa moyo mmoja, ndugu zangu tusafishe
 3. Tujaze kifusi penye ubinafsi, tusafishe tusafishe
  Tujenge upendo kwa jamii yote, tusafishe tusafishe
  Tusafishe bila ya kinyongo, ndugu zangu tusafishe
  Tusafishe kwa moyo mmoja, ndugu zangu tusafishe
 4. Penye fitina tumwage Molami, tusafishe tusafishe
  Penye majungu tumwage Molami, tusafishe tusafishe
  Tusafishe bila ya kinyongo, ndugu zangu tusafishe
  Tusafishe kwa moyo mmoja, ndugu zangu tusafishe
 5. Tuzisafisheni nyumba za wachawi, tusafishe tusafishe
  Tuzisafisheni kwa jina la Mungu, tusafishe tusafishe
  (ii) Tusafisheni kwa imani, ndugu zangu tusafishe
  Tusafishe siku ile yaja, ndugu zangu tusafishe
 6. Tuing'oeni mizizi ya vita, tusafishe tusafishe
  Tupalilie shamba la upedo, tusafishe tusafishe
  (ii) Sisi sote ni watoto wa Mungu, ndugu zangu tupendane,
  Sisi sote baba yetu mmoja, ndugu zangu tupendane.
Hii ni Sauti
COMPOSERE. F. Jissu
CHOIRKwaya ya Moyo Safi wa Bikira Maria, Unga Limited Arusha
ALBUMMilele Milele Nitakusifu
CATEGORYMajilio (Advent)
 • Comments