Mbinguni ni Furaha Lyrics

MBINGUNI NI FURAHA

@ JohnBosco Hosea

 1. Nimeahidiwa utukufu mbinguni – Kwake Mungu Baba
  Nikamilishapo kazi yake Bwana – Aliyeniumba
  Nitatunukiwa tuzo za kifalme – nikiwa mshindi

  {t/b} Mbinguni ni furaha
  Tutaimba, na kucheza
  Tutaruka kwa furaha tukimwona Mungu,
  Tuendapo paradiso aliyotuandalia sisi wateule x2

 2. Nyimbo za ushindi mimi nitaimba – Nikimwona Mungu
  Sauti za mbinguni mimi nitapewa – naye Mungu wangu
  Nikiwa na kwaya tamu za malaika – wote wa mbinguni
  Tutaimba hosanna
 3. Makao ya kifahari mimi nitapewa – nilioandaliwa
  Yaliyo na urembo usio na mifano – ya dhamani kubwa
  Mandhari ya dhahabu na pia almasi – yanayometemeta
  Mbinguni kwapendeza.
 4. Nitashangilia nikiwa barazani – pamoja na Mungu
  Na watakatifu wake Mungu Baba – walionitangulia
  Karamu ya wateule tutaandaliwa – kufutwa machozi,
  Kwa shangwe na nderemo.
 5. Makao ya kifahari kweli ni mazuri – tena matulivu,
  Yasiyo na njaa shida wala kifo – furaha kila siku,
  Kazi ni kumsifu na kutukuza Mungu – milele amina
  Huko ndiko nyumbani.
Mbinguni ni Furaha
COMPOSERJohnBosco Hosea
ALBUMUwe Nami Bwana
CATEGORYTafakari
 • Comments