Tazama Ninakuja Kwako Lyrics

TAZAMA NINAKUJA KWAKO

@ JohnBosco Hosea

Tazama ninakuja kwako (Bwana),
Niyafanye mapenzi yako
Mimi ninajitoa kwako,
naja kwako Bwana nipokee x2

 1. Nimesikia Bwana, sauti yako yaniita kwako,
  Yaniita nije kwako ili nikakutumikie.
  Na mimi sina budi, kuitika wito wako,
  Maana kila siku mimi hukutafuta wewe.
 2. Naja kwako Bwana, nimejawa na furaha tele,
  Nafsi yangu yashangilia kwa kuikaribisha kwako.
  Na moyo wangu Bwana unakutukuza wewe,
  Maana wastahili sifa zote pia utukufu.
 3. Tazama naja kwako, ninayaleta maombi yangu,
  Na sala zangu zote ninakuomba uzipokee.
  Unisamehe dhambi na maovu niliyoyatenda,
  Ili mimi niwe tayari kukupa sadaka takatifu
 4. Ninajitoa kwako kuyatenda mapenzi yako,
  Kwa nguvu zangu zote, kwa mawazo pia kwa vitendo,
  Unijalie heri, unipe Roho Mtakatifu,
  Aniongoze mimi, nitimize ninayoahidi.
Tazama Ninakuja Kwako
COMPOSERJohnBosco Hosea
ALBUMUwe Nami Bwana
CATEGORYInjili na Miito (Gospel)
 • Comments