Ee Mungu Nitakutafuta Mapema Lyrics

EE MUNGU NITAKUTAFUTA MAPEMA

@ JohnBosco Hosea

[ t ] Ee Mungu, mungu wangu ee Bwana
[ w ] Nitakutafuta mapema, nafsi yakuonea kiu x2
[ t ] Maana
[ w ] Maneno yako ni Roho na uzima
Wewe unayo maneno ya uzima wa milee x2

 1. [ s ] Ee Mungu, Mungu wangu, nitakutafuta mapema,
  Nafsi yakuonea kiu, mwili wakuonea shauku,
  Kwenye nchi kavu yenye uchovu,
  Nchi kavu isiyo na maji.
 2. [ t ] Ndipo nilikutazama, katika patakatifu,
  Nizione nguvu zako, na utukufu wako,
  Maana fadhili zako, ni njema kuliko uhai,
  Nafsi yangu itakusifu.
 3. [ a ] Ndipo nitakubariki, wakati mimi naishi,
  Nikiinua mikono yangu, nitaliomba jina lako,
  Kwa utajiri wa karamu, nafsi yangu imeridhika,
  Kwa midomo ya kinywa changu, nitakusifu wewe.
 4. [ b ] Wewe ni msaada wangu,
  Katika uvuli wa mbawa zako, hupiga kelele kwa furaha.
  Nafsi yangu hushikamana, haraka kwako Bwana,
  Kwa midomo ya kinywa cha-a-ngu, nitaku-usifu wewe.
Ee Mungu Nitakutafuta Mapema
COMPOSERJohnBosco Hosea
CHOIRSt. Monica Lower Kabete Campus UoN
ALBUMUwe Nami Bwana
CATEGORYZaburi
 • Comments