Sikuifukia Talanta Yangu Lyrics

SIKUIFUKIA TALANTA YANGU

@ Victor Aloyce Murishiwa

Sikuifukia talanta yangu, tazama Bwana naleta kwako leo
Ninaleta shukrani zangu pokea Baba, ni mali yako

Hivi vyote ni vyako, (mimi) nimepata kwa wema wako
nasema asante Baba, asante, asante, asante * 2

  1. Umenijalia nguvu na akili, nikazitenda kazi
    Nimepata riziki zangu asante Baba asante
  2. Umenijalia siku za furaha nami nikafurahi
    Nikasifu jina la Bwana asante Baba asante
  3. Umemtoa mwanao Yesu Kristu aje kunikomboa
    Katika utumwa wa dhambi, asante Baba asante
Sikuifukia Talanta Yangu
COMPOSERVictor Aloyce Murishiwa
CATEGORYOffertory/Sadaka
MUSIC KEYG Major
TIME SIGNATURE2
4
NOTES Open PDF
  • Comments