Ninataka Kuingia

Ninataka Kuingia
Performed by-
CategoryKwaresma na Toba (Lent & Repentance)
Views21,905

Ninataka Kuingia Lyrics

  1. Ninataka kuingia, mjini mwa Mungu
    Nitashinda nitakaza mwendo nifike
    Nikishikwa na shida, nikichoka njiani
    Yesu unaniambia uningojee
  2. Naitwa na Yesu Kristu enzini mwake
    Nakimbia kukawia hakuna faida
    Wote wachelewao hawatapata taji
    Mimi sitaki kingine ila uzima
  3. Elekeza macho yangu mlangoni pako
    Niongoze nipe nguvu nikilemewa
    Ninapojaribiwa, ninaposingiziwa
    Yesu unisaidie nisikuache
  4. Mkono wako unishike nisianguke
    Najiona kuwa mnyonge nguvu i kwako
    Neno lako ee Yesu linanipa uzima
    Nikifika nitaimba umeniponya
* nikilemewa - some versions sing "ninapochoka"