Bwana Roho Zetu Lyrics

BWANA ROHO ZETU

 1. Bwana roho zetu zatamani, hayo maji yenye uzima
  Bwana roho zetu zina kiu, tupe maji hayo ya uzima.

  Ee Bwana, tuna kiu, tunyweshe, tuna kiu
  Ee Bwana, tupe maji hayo ya uzima *2

 2. Wewe ndiwe taa ya maisha, wewe Ndiwe mweza vyote.
  Wewe ndiwe mwanga wetu sote, utatuongoza daima.
  Ee Bwana, tunajua daima tuko nawe.
  Ee Bwana, utatuongoza daima *2
 3. Wewe ndiwe nguvu yetu sote, wewe ndiwe mweza vyote.
  Tupigwapo kumbo na shetani, wewe ndiwe tulizo letu.
  Ee Bwana, tuongoze daima maishani.
  Ee Bwana, tupe nuru yako njiani *2
Bwana Roho Zetu
CATEGORYEkaristia (Eucharist)
 • Comments