Bwana Yesu Fadhili Zako Lyrics

BWANA YESU FADHILI ZAKO

 1. Bwana Yesu, fadhili zako ni za milele
  Uaminifu wako kwetu wadumu milele.

  Mwi- Mwimbieni Bwana,
  Mshu- Mshukuruni Bwana,
  Imbeni aleluya Bwana,
  Tukumbuke rehema zake. *2

 2. Bwana Yesu, fadhili zake ni za milele
  Mwili wako posho safarini kwa milele.
 3. Bwana Yesu, fadhili zako ni za milele
  Damu yako yatufikisha hadi milele.
 4. Bwana Yesu, fadhili zako ni za milele
  Watupenda sisi kwa upendo wa milele.
 5. Aleluya, mataifa, musifuni Bwana,
  Enyi watu wote mwimbieni na kumkuza.
Bwana Yesu Fadhili Zako
CATEGORYThanksgiving / Shukrani
 • Comments