Mwamba Wenye Imara

Mwamba Wenye Imara
Performed by-
CategoryKwaresma na Toba (Lent & Repentance)
Views45,512

Mwamba Wenye Imara Lyrics

  1. Mwamba wenye imara, kwako nitajificha
    Maji hayo na damu, yaliyo toka humu
    Hunisafi na dhambi, hunifanya mshindi
  2. Kwa kazi zote pia, sitimizi sheria
    Nijapofanya bidii, nikilia na kuudhi
    Hayaishi makosa, niwe wa kuokoa
  3. Sina cha mkononi, naja msalabani
    Nilitupu, nifike, ni mnyonge, nishike
    Nilimchafu naja, nioshe nisijafa
  4. Nikungojapo chini, na kwenda kaburini,
    Nipaapo mbinguni, na kukwona enzini
    Roho yangu naiwe, rahani mwako wewe