Nasikia Yesu Waniita

Nasikia Yesu Waniita
Performed by-
CategoryEkaristia (Eucharist)
Views13,286

Nasikia Yesu Waniita Lyrics

  1. Nasikia Yesu waniita, kwa mlio wa neema yako
    N'tawezaje bado kusita, wako kufuata mwaliko

    Yesu wataka nikupende, nifumbue wako moyo
    Kujificha ndanie, niende nionje tamu rahayo

  2. Sheria yako tamu, nzuri, kwa upole wako
    Yafaa kushika zako zote amri aweza nani kukataa
  3. Wa roho niwie mwalimu, mwake ujifumbulie.
    Kukujua nipe elimu, Yesu mwema nijalie
  4. Wa Mungu moyo udhaifu, kukukasirisha.
    Ee moyo safi, mtakatifu, sitakukosa zaidi.
  5. Niwezeshe na malaika kisha acha mwili wangu
    Kukusifu Rabi hakika na kuonja heri ya mbingu