Nipokee Bwana Nipokee Lyrics

NIPOKEE BWANA NIPOKEE

@ (traditional)

 1. Nipokee, Bwana wangu, nipokee,
  Mbele zako nipo daima,
  Sinitupe mbali nawe miye mdhambi,
  Nipokee, Bwana wangu nipokee.
 2. Nakupenda Yesu mwema, nakupenda,
  Kwa hiari yako U name,
  Usinione kosa langu, nisamehe,
  Nakupenda, Yesu mwema, nakupenda.
 3. Uje kwangu, Yesu mwema, uje kwangu,
  Tumaini langu ni kwako,
  Vya dunia hudanganya, huumiza,
  Uje kwangu, Yesu mwema, uje kwangu.
 4. Siondoke, Yesu mwema, siondoke,
  Nisiachiliwe gizani,
  Kaa nami, moyo wangu wakutaka,
  Siondoke, Yesu mwema, siondoke.
 5. Ninakupa mali yangu, ninakupa,
  Ona ninakurudishia,
  Nifundishe kutumia vyote kwako,
  Ninakupa mali yangu, ninakupa.
Nipokee Bwana Nipokee
COMPOSER(traditional)
CATEGORYInjili na Miito (Gospel)
 • Comments