Twendeni Wote Kwa Bwana Lyrics

TWENDENI WOTE KWA BWANA

Twendeni wote kwa Bwana,
Atualika karamuni,
Tukale mkate wa mbingu.

 1. Yeye mwenyewe ni Mungu,
  Na pia ni mwanadamu, jamani.
 2. Yeye ni mkate halisi,
  Yeye ni shibe halali, jamani.
 3. Yeye ni Mwana wa Mungu,
  Mtawala Mkuu wa mbingu, Jamani.
 4. Yeye ni penzi la Baba,
  yeye ni Neno la Baba jamani.
 5. Yeye ni mwanga wa kweli,
  Tena ni njia ya kweli, jamani.
 6. Yeye ni mpenzi wa wote,
  faraja kweli kwa wote, jamani.
 7. Yeye ni mlango wa mbingu,
  Tuzo na heri ya mbingu, jamani.
Twendeni Wote Kwa Bwana
CATEGORYEkaristia (Eucharist)
 • Comments