Bwana ni Mchungaji Lyrics

BWANA NI MCHUNGAJI

@ Reuben Kagame

 1. Bwana ni mchungaji wangu,
  Sitapungukiwa kitu
  Hun’laza penye majani mabichi,
  Huniongoza kwa maji matulivu

  Hakika wema nazo fadhili zitanifuata mimi,
  Nitakaa nyumbani mwa Bwana,
  Siku zote za maisha yangu

 2. Hunihuisha nafsi yangu,
  Hun’ongoza kwa njia za haki
  Nipitapo bondeni mwa mauti,
  Sitaogopa wewe u nami
 3. Gongo lako na fimbo yako,
  Vitanifariji mimi
  Waandaa meza mbele yangu,
  Machoni pa watesi wangu
Bwana ni Mchungaji
COMPOSERReuben Kagame
CATEGORYZaburi
REFZaburi 123
 • Comments