Mtafuteni Bwana Lyrics

MTAFUTENI BWANA

(Mtafuteni Bwana) maadamu anapatikana
(Mwiiteni Bwana wenu) Maadamu yu karibu
{Mtu mbaya na aache njia yake ya upotovu,
Asiye haki amrudie Bwana asamehewe } *2

 1. Bwana Mungu asema mawazo yangu mimi kweli si mawazo yenu,
  Wala njia zangu sio njia zenu maana mimi Mungu wenu *2
 2. Heri wanaozingatia matakwa yake, wamtafutao,
  kwa moyo wote, watu wasiotenda uovu wala udhalimu
 3. Ninakutazama kwa hamu Mungu wangu, mtawala wangu kinga,
  nguvu zangu,nitakuhimidi ninapokutegemea
 4. Angalia mateso yangu niokoe Mungu, unitetee
  Mungu nijalie uhai uwe nami daima maana nakutumaini.
Mtafuteni Bwana
CATEGORYZaburi
REFIsaya 55
 • Comments