Enda Nasi Bwana

Enda Nasi Bwana
Performed by-
CategoryRecession
ComposerReuben Kagame
Views46,339

Enda Nasi Bwana Lyrics

  1. Tunaomba uwepo wako uende nasi
    Ewe Bwana wa majeshi tusikie
    Kama huendi nasi, hatuwezi kutoka hapa
    Hatuwezi peke yetu, enda nasi
  2. Tu watu wa shingo ngumu tusamehe
    Hatufai mbele zako turehemu
    Tusafishe ee Baba, tuonyeshe uso wako
    Twahitaji neema yako enda nasi

    Tutavua mapambo yetu,
    Vitu vyote vya thamani kwetu
    Mioyo yetu twaleta mbele zako
    Tutakase na utembee nasi .

  3. Tunaomba utuonyeshe njia zako,
    Kwa maana umetuita kwa jina lako,
    Twalilia ee Bwana, utukufu na uso wako
    Bila wewe tutashindwa enda nasi