Kifua Mbele

Kifua Mbele
Performed by-
CategoryTBA
ComposerRenatus Rwelamira
Views2,463

Kifua Mbele Lyrics

  1. Natembea kifua kikiwa mbele mimi
    Natembea kifua kikiwa mbele mimi
    Sina hofu kamwe moyoni mwangu
    Kwa kuwa nina Yesu moyoni mwangu mimi
    {Niacheni niimbe, niacheni nicheze
    Niacheni niruke, nimsifu Mungu wangu } *2
  2. Ni yeye Mungu wangu, mimi nitamsifu
    Na ndiye Muumba wangu, mimi nitamwimbia
    Nitamsifu Mungu wangu kila niamkapo
    Nitamwimbia nyimbo tamu tena za kupendeza
    iyelelele iyele
  3. Yeye ndiye mlinzi wangu, mlinzi mwaminifu *2
    Yeye ni Alfa tena yeye ndiye Omega * 2
    iyelelele iyele
  4. Nitamshukuru Bwana kwa moyo wangu
    Nitayasimulia matendo yake yote
    Nitafurahi na kushangilia wewe Bwana
    Nitaliimba jina lako wewe uliye juu