Shangilia Harusi

Shangilia Harusi
Performed by-
CategoryHarusi
Views3,680

Shangilia Harusi Lyrics

  1. Yelele lele, yelele lele, leo tunayo furaha tele tele
    Twasherehekea arusi ya wenzetu
    Wamejitolea kwa moyo wao wote
    Twasherehekea yote wametimiza
    Arusi leo shangilia aa, shangilieni maarusi hawa
    Arusi leo furahia aa, furahieni maarusi hawa

  2. Twaombea baraka zake Bwana
    Munapoanza maisha haya mapya
    Shetani asiwatenganishe kamwe
    Mubaki ndani ya Bwana Mungu wetu
  3. Ewe mwanaume umpende mke wako
    Kwani hiyo ndiyo amri ya Mungu wetu
    Nawe mwanamke umpende mume wakao
    Ndipo ndoa yenu isimame imara
  4. Msiwasahau wazazi wenu pia
    Kwani hao ndio nguzo ya masha yenu
    Watoto wenu na muwatunze vema
    Muwapeleke kwa kanisa ya Bwana
  5. Na sisi sote tulioshuhudia
    Arusi yenu siku hii ya leo
    Twawahimiza mheshimu ndoa yenu
    Kwani ndoa ni sakramenti takatifu

    Yelele lele, yelele lele
    Shangilieni maharusi hawa, furahieni maharusi hawa