Waipeleka Roho Yako Lyrics

WAIPELEKA ROHO YAKO

Waipeleka Roho Yako ee Bwana
Nawe waufanya upya uso wa nchi
Waipeleka Roho Yako ee Bwana
Nawe waufanya upya uso wa nchi

 1. Ee nafsi yangu umhimidi Bwana
  Wewe Bwana Mungu wangu umejifanya mkuu sana
  Ee Bwana jinsi yalivyo mengi matendo yako
  Dunia imejaa mali zako
 2. Waiondoa pumzi yao wanakufa
  Na kuyarudia mavumbi yao
  Waipeleka Roho yako wanaumbwa
  Nawe waufanya upya uso wa nchi
 3. Utukufu wa Bwana na udumu milele
  Bwana na ayafurahie matendo yake
  Kutafakari kwangu na kuwe kutamu kwake
  Mimi nitamfurahia Bwana
 • Comments