Nimemwacha Wapi Bwana Lyrics

NIMEMWACHA WAPI BWANA

@ E. A. Minja

 1. Mimi ni kitu gani na niko wapi, ninatoka wapi
  Ninakwenda wapi, mimi nimemwacha Bwana wangu nimtumainiaye
  Kaniumba kanitofautisha na wanyama kwa utashi
  Ndiye anayeitegemeza nafsi yangu mchana usiku hunilinda

  {Nimemwacha wapi (Bwana) Bwana wangu
  mimi naenda kujiongoza
  Imani yangu imekuwa nia tu siku hadi siku
  Matendo yangu yamekuwa ni kinyume toka kitambo
  Kwa ajili hii ona ninafanya kazi
  na kujinyima nafsi yangu mema } *2

 2. Maisha yangu ni safari tangu kuumbwa kuzaliwa
  Na kuishi kwangu hapa duniani mwisho nipate uzima wa milele
  Yeye anipaye pumzi ya uhai wangu na mlinzi wa maisha yangu
  Kwa kila hatua ya maisha yangu hapa duniani
 3. Kanisani nakwenda natoa sadaka na zaka
  Lakini ulevi mimi unanitawala kwani pombe ndiye wangu mfariji
  Anasani maishani yake na ya famili yake
  Na gizani uzinzi ni wangu rafiki sakramenti ya ndoa iko wapi
 4. Watoto wapatao mali kwa mganga kupiga bao
  Nyumba nayo izindikwe hirizi, mikononi nami urogi kaurithi
  Kutosita hio nihoji ndugu na jirani
  Ati jirani yule ndiye jina fulani nikimsema kusengenya napenda
 5. Maana sheria zako ni kama kioo mbele ya matendo yangu,
  Moyo wangu wanielemea nikitafakari matendo yako
  Maana sheria zako ni kama kioo mbele ya imani yangu,
  Maisha yangu yamekuwa gizani tena ni maisha ya dhambi
 6. Ewe ndugu yangu jiulize moyo wako uko wapi
  Na matendo yako yampendeza Muumba wako kwa uzima alokupa
  Ewe Baba mama vijana ewe mlei hebu jiulize
  Mwisho wa maisha yako haya utaupata uzima wa milele
Nimemwacha Wapi Bwana
COMPOSERE. A. Minja
CATEGORYTafakari
 • Comments