- Tunakuwa tunasinzia hatujitambui
Tunaamka tunajikuta tungali haiFuraha furaha furaha furaha
Bwana Yesu furaha shangwe na chereko
na furaha, furaha furaha sana
- Mawio mpaka macheo huambatana nasi
Usiku nguzo ya moto na mchana ya wingu
- Kwenye machozi muda wote tunalia naye
Anatuinua mkono tukacheka naye
- Tunapoondokewa na ndugu zetu wachache
Anatupa tumaini kuwapokea kwake
- Tunajivuna kwa sababu tunaye Mungu
Tunamuomba awe nasi daima milele
|
Recorded also by St. Don Bosco Kyaani Mombasa
|
|