Tawi Limechipuka Lyrics

TAWI LIMECHIPUKA

 1. Tawi limechipuka shinani mwa Yesu
  Kama tulivyopashwa habari na wazee
  Likatoa ua, wakati wa usiku, lililochanua
 2. Isaya alitaja ua hilo zuri
  Ni Yesu mponya wetu, Maria alimzaa
  Usiku mtulivu, uwezo wake Mungu, umefanya hivi
 3. Na ua hili dogo lanuka vizuri
  Lang'aa kama jua, giza lafukuza
  Ni Mwana wa Mungu, hata mwana Adamu, Mwokozi wa watu
 4. Siku ya kufa kwetu, Yesu tuongoze
  Tuiache dunia, twende furahani
  Mbinguni kwa Mungu, pale tutakusifu, milele daima
Tawi Limechipuka
CATEGORYNoeli (Christmas Carols)
 • Comments