Bwana Mungu Aliona Lyrics

BWANA MUNGU ALIONA

 1. Bwana Mungu aliona Mwanakondoo apotea
  Kwa upendo akamtoa Mwana wake wa pekee

  Alelu - aleluya kazaliwa
  Yesu mwa - Yesu Mwana wa Pekee
  Bethlehe - Bethlehemu amelazwa
  Mama - Mamayo Maryamu

 2. Lile neno lilikuwa maandishi yanenavyo
  Na kwa yeye vitu vyote vikapata kuwepo
 3. Siku Yesu alizaliwa watu wote walishangilia
  Wakasema huyu mfalme Mwokozi wa dunia
Bwana Mungu Aliona
CATEGORYNoeli (Christmas Carols)
 • Comments