Ni Kweli Amezaliwa

Ni Kweli Amezaliwa
Performed by-
CategoryNoeli (Christmas Carols)
ComposerA. Liampawe
Views3,517

Ni Kweli Amezaliwa Lyrics

  1. Ni kweli amezaliwa Mkombozi wetu Masiha
    Malaika wanaimba kwa furaha wakimsifu Bwana
    {Na sisi tunafurahia Mkombozi wetu kazaliwa
    Na utumwa umetutoka aleluya tushangilie } *2

  2. Kwenye mji wa Daudi Mkombozi kazaliwa
    Wote twende tukamwone amelazwa manyasini
  3. Tuna haki kufurahi tumepata Mkombozi
    Amekuja tukomboa hivyo wote tufurahi
  4. Utukufu juu Mbinguni, na amani duniani
    Kwa watu wote wenye mapenzi mema aleluya
  5. Bwana Yesu kazaliwa, amekuja tukomboa
    Katuletea wokovu, hivyo tuimbe aleluya