Lala Kitoto cha Mbingu Lyrics

LALA KITOTO CHA MBINGU

@ D. Mlolwa

Lala kitoto cha Mbingu, lala sinzia lala
Malaika wake Mungu atakutunzia
Lala kitoto cha Mbingu, lala sinzia lala
Malaika wake Mungu atakutunzia

{ Lala (kitoto) lala lala (sinzia) lala (sinzia)
Lala kitoto lala sinzia Mwana wa Mungu }*2

 1. Lala kitoto lala, sinzia mtoto
  Malaika wa Mungu atakutunzia
  Lala Mwana wa Mungu, Mungu wetu sinzia
  Malaika wake Mungu atakutunzia
 2. Maria na Yusufu, wambusu kitoto
  wachungaji wanapiga magoti kusujudia
  Ni mfalme wa amani, mshauri wa amani
  Mungu Mwenyezi Baba yetu, wa milele milele
 3. Nasi twendeni hima, tukamwone mtoto
  Tumsalimie yeye, pamoja naye Mama Maria
  Tumsujudie Mfalme, tumtolee zawadi,
  Ndiye Mkombozi aliyekuja, kwa ajili yetu sisi
Lala Kitoto cha Mbingu
COMPOSERD. Mlolwa
CHOIRSt. Peter Oysterbay
ALBUMNyimbo za Noeli
CATEGORYNoeli (Christmas Carols)
SOURCETanzania
 • Comments