Hodi Wachunga Lyrics

HODI WACHUNGA

@ (traditional)

 1. Hodi wachunga, msiwe na woga
  Amkeni upesi, Bethlehemu mje nasi
  Alipozaliwa Mwokozi wenu
 2. Haya twendeni, yumo pangoni
  Nyasi alalia alowashukia
  Mwenyeji wa mbingu Mwokozi wenu
 3. Pamoja naye mna mamaye
  Yeye na Yosefu, mlinziwe mtukufu
  Wamtunza kitoto, Mwokozi wenu
 4. Mtukufu Mungu katika mbingu
  Na kwenu amani kwa watu amani
  Wenye kumwungama Mwokozi wenu
 5. Wakristu nyie twende na siye
  Kwenye mwana mchanga kama`o wachunga
  Nasi tumwabudu Mwokozi wetu
Hodi Wachunga
COMPOSER(traditional)
CATEGORYNoeli (Christmas Carols)
MUSIC KEYD Major
TIME SIGNATURE4
4
SOURCETraditional
NOTES Open PDF


Recorded by
* St. Cecilia
* St. Cecilia Mavurunza
 • Comments