Kimya Bara na Bahari

Kimya Bara na Bahari
Performed by-
CategoryNoeli (Christmas Carols)
ComposerFr. G. F. Kayeta
Views6,105

Kimya Bara na Bahari Lyrics

  1. Kimya bara na bahari, kimya mbingu na dunia
    Bwana na Muumba wenu, mtoto Yesu asinzia

    Kimya, kimya, asinzia, mpenzi wetu mtoto Yesu * 2

  2. Amelazwa manyasini, mchanga mkiwa, myonge pia
    Yosefu na Maria wamo, mtoto Yesu kumtunzia
  3. Malaika wanashuka, mfalme wao kumlindia
    Wanatunga nyimbo nzuri, mtoto Yesu kumwimbia
  4. Wachungaji waja mbio, kwa mshangao waingia
    Waanguka magotini, mtoto Yesu kumuabudia
  5. Nasi pia twende hima, Mungu wetu kumwangalia
    Twende sote kwa juhudi, mtoto Yesu kumwamkia
St. Cecilia