- Malaika kaleta Noeli ya kwanza,
Kwa wachunga kondoo katika makonde,
Bethlehemu wakawa walinzi wa zamu,
Wakaona usiku ajabu ya nuru{ Noeli, Noeli, Noeli, Noeli,
Yesu yu Mungu na binadamu } *2
- Wakaona mbinguni, mwangaza wa nyota,
Ing'aayo kwa mbali na masharikini,
Wakaenda upesi, walivyoambiwa.
Bethlehemu wamwone Mwokozi horini
- Mashariki watoka wafalme watatu,
Mamajusi waliotafuta mfalme,
Wafuata hii nyota waliyoiona,
Wasipate kumkosa wanayemtafuta
- Kiongozi ni nyota iliyowaleta
Hata mji wa Daudi alimozaliwa
Ikakaa mara moja isiendelee
Pale pale nyumbani alimo Mwokozi
- Mamajusi walipoingia nyumbani
Wakapiga magoti kwa heshima kuu
Mara hiyo walipozifungua hazina
Manemane, uvumba, dhahabu, watoa
- Basi sisi wakristu na tumsujudie
Tumhimidi Mwokozi, aliyeviumba
Vitu vyote mbinguni duniani na sisi
Na ametufia na kutukomboa
|
* St. Peter Osterbay * St. Cecilia
The First Noel
|
|