Ya Nini Malumbano

Ya Nini Malumbano
Performed by-
CategoryTBA
ComposerVictor Aloyce Murishiwa
Views3,457

Ya Nini Malumbano Lyrics

  1. {Ya nini malumbano hayo
    Ya nini malumbano hayo ndani ya moyo wako} *2

    Chagua kuwa moto au baridi sio vuguvugu
    ewe Mkristu utaponea wapi wewe
    Chagua kuwa moto au baridi sio vuguvugu
    ewe Mkristu utaponea wapi wewe

  2. Asubuhi kanisani na jioni kwa waganga
    Siku ya mwisho utaponea wapi wewe
    Yesu unamhitaji na dunia unaipenda
    Siku ya mwisho utaponea wapi wewe
  3. Imani bila matendo haifai kitu kwa Bwana
    Siku ya mwisho utaponea wapi wewe
    Angalia wadhulumu maskini na wahitaji
    Siku ya mwisho utaponea wapi wewe
  4. Uongo unaongea kutwa kucha wala huchoki
    Siku ya mwisho utaponea wapi wewe
    Rushwa unapokea majivuno wala huachi
    Siku ya mwisho utaponea wapi wewe