Hazina ya Mvivu ni maneno ya uongo (na tena)
Furaha ya mvivu ni kugombanisha watu
- Hawezi kulala kapata usingizi usiku
Usiku mzima hukodoa macho akiwaza
Kukipambazuka aende kwa nani kupiga umbeya
- Asubuhi mapema huamka na kuvaa nguo
Hajafagia nyumba huyo huyo kwa jirani kaenda
Hodi jirani jirani naye karibu tupo unasemaje
Atapiga umbea hapo hadi chakula cha mchana ale
- Akipitapita mitaani huwa amependeza
Salamu kwa watu utasema huyu ni mtu mwema
Kumbe ni muovu asiye kuwa na aibu kwa watu
- Wenzake wanaamka mapema na kwenda kazini
Yeye akiamka huyo huyo safari kwenye pombe
Akishafika huko tazama anavyolewa wala hawazi
Familia yake itakula nini mchana na usiku
|
|
|