Asubuhi na Mapema

Asubuhi na Mapema
Performed by-
CategoryTBA
Views5,130

Asubuhi na Mapema Lyrics

  1. Asubuhi na mapema, siku ya kwanza ya juma
    Wanawake walikwenda kaburini
    Wakiwa na mafuta na manemane
    Ili wampake Bwana ilivyo desturi *2

    Pale kaburini walishikwa na mshangao
    Kaburi li wazi hafungwi
    Mwokozi ametoka mzima
    Kafufuka alivyosema

  2. Kufika pale kaburini, waliona li wazi
    Wakabaki wakilia, ati Bwana wamemchukua
  3. Jiwe lilikuwa kando, ndani vimo vitambaa
    Alivyofunikwa Bwana, kweli Bwana amefufuka
  4. Tufurahi watu wote Bwana wetu kafufuka
    Katuondolea dhambi kweli tuimbe aleluya